Baada ya kukwama jijini Mwanza, hatimaye wachezaji watano wa Simba, wameungana na wenzao mjini Bukoba.
Simba inajiandaa kuivaa Kagera Sugar kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
Kabla ya kuungana na wenzao mjini humo walilazimika kulala jijini Mwanza baada ya mvua kubwa zilizonyesha mjini Bukoba kusababisha uwanja wa ndege kujaa maji.
Kujumuika kwa wachezaji hao, kunaifanya Simba iwe imeongeza nguvu ya wachezaji watano waliokuwa katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kilichonyoa Morocco kwa mabao 3-1.
Hata hivyo, mmoja wao, Mwinyi Kazimoto ameachwa jijini Dar es Salaam na imeelezwa kwamba kocha Patrick Liewig amekuwa hafurahishwi na mwenendo wake.
Simba inahitaji ushindi katika mchezo huo wa ugenini ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kupambana na Yanga na Azam FC.
Simba ambao ni mabingwa watetezi wanaonekana kupoteza mwelekeo katika kuwania kutetea taji lao hilo la Ligi Kuu Bara.
Pamoja na kuwa katika wakati mgumu, Simba imekuwa ikisisitiza kutumia kikosi cha wachezaji vijana huku 'masupastaa' kibao wakipigwa chini.
0 COMMENTS:
Post a Comment