Baada ya kuonyesha cheche zao, washambuliaji wawili Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu watakuwa na kibarua kingine Jumapili.
Samatta na Ulimwengu walionyesha uwezo mkubwa na kufanikiwa
kuiongoza Stars kupachika mabao 3-1 dhidi ya Morocco Jumapili iliyopita.
Wawili hao watakuwa na kibarua kingine kigumu dhidi ya Saint
Eloi Lupopo wakati watakapokuwa wanaichezea klabu yao ya TP Mazembe.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya DR Congo inasumbiriwa kwa hamu
kutokana na upinzani mkubwa wa timu.
Timu hizo zimekuwa na upinzani mkubwa kutokana na kuwa
majirani, hivyo Samatta na Ulimwengu watatakiwa kudhihirisha tena kwamba
wlaichofanya Dar es Salaam hawakubahatisha.
Mechi hiyo itaanza saa 9:30 Alasiri kwa saa za Afrika ya Kati,
itakuwa saa 10:30 jioni kwa Afrika Mashariki.
Samatta amekuwa kati ya wafungaji wanaotegemewa katika kikosi
cha TP Mazembe, wakati Ulimwengu anachukuliwa kama wachezaji wanaochipukia na
faida ya baadaye.
0 COMMENTS:
Post a Comment