KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Adel
Amrouche amesema huu ndiyo wakati wa Afrika Mashariki kucheza Kombe la Dunia.
Amrouche ambaye alikuwa kocha wa Burundi, amesema ushindi wa
Tanzania dhidi ya Morocco na sare ya Kenya dhidi ya Nigeria, tena ikiwa ugenini
ni dalili kwamba kuna timu inaweza kufika mbali na kucheza Kombe la Dunia.
Akizungumza kutoka Nairobi, Amrouche alisema huu ndiyo wakati mwafaka wa kujiamini kwamba inawezekana na ndiyo kipindi mwafaka cha mapinduzi kwa Afrika Mashariki na Kati.
“Mpira wa Afrika hauna tofauti kubwa katika kipindi hiki,
kuna kila sababu ya watu wa ukanda huu kuamini wenzetu wametangulia lakini
tunaweza kufanya mabadiliko.
“Nigeria walibahatisha kusawazisha dhidi yetu baada ya
kupoteza umakini pia, lakini Tanzania imefunga Morocco mabao matatu, pia
imeonyesha uwezo mkubwa.
“Hakika tunaweza, hatupaswi kujirudisha nyuma. Lazima tujiamini
na inawezekana kati ya nchi za ukanda huu, moja ikapata nafasi Kombe la Dunia,”
alisema Amrouche, raia wa Ubeligiji mwenye asili ya Algeria.
Kenya ilitoka sare ya bao 1-1 na Nigeria huku ikiwa ugenini,
wenyeji hao walilazimika kusawazisha wakati wa dakika nne za nyongeza wakati
Stars iliichapa Morocco bao 3-1.
Timu nyingine ya ukanda huu iliyoshinda ni Ethiopia, ikiwa
nyumbani ikaitwanga Botswana 1-0, Uganda wakalala 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya
Liberia na Sudan ikafumuliwa 4-0 na wenyeji wake Ghana.
0 COMMENTS:
Post a Comment