March 16, 2013





FULL TIME: Mwamuzi anapuliza kipenga cha kumaliza mpira, Yanga inatoka kifua mbele kwa bao moja.
Dk 90, Shooting wanaonekana kuchanganyikiwa, Yanga wanafanya shambulizi la kushitukiza. Nusura Msuva afunge bao la pili.
 Dk 83 Ruvu inamtoa Ayoub Kitala ameingia Raphael Kyala, bado inaonekana hakuna tofauti kubwa sana.
Dk 80, Luhende aliyeingia kuchukua nafasi ya Oscar, anatoa pasi nzuri kwa Msuva lakini anashindwa kuwa makini kumalizikia karibu kabisa na lango la Shooting.


Dk 75, Nizar anajaribu kupiga shuti lakini Mangasi anamuwekea mguu na kumuumiza, inaonekana hataendelea. Anatolewa na nafasi yake anachukua Kavumbagu.


Dk 71, pasi nzuri ya Juma Abdul inafikia Nizar kichwani, lakini anashindwa kulenga, mpira unatoka.

Dk 70 Shooting wanafanya shambulizi zuri lakini umakini wa Dilunga unakuwa mdogo.



Dk 57 Kiiza anaumia baada ya kugongana na beki wa Shooting, mpira unasimama kwa zaidi ya dakika mbili.



Dk 56 Ruvu wanafanya mabadiliko, ametoka Gideon Tepo ameingia Paul Ndauka
Dk 54, Kiiza angeweza kufunga bao la pili baada ya pasi nzuri ya Nizar, lakini anapiga kichwa kama anaokoa.

GOOOOOOOO...Dk 48, Kiiza anaifungia Yanga bao baada ya pasi nzuri ya kuinua juu ya Nizar, naye anamchambua kipa Haule.

Dk 46, Yanga wanafanya shambulizi kali lakini mabeki wa Shooting wanaondosha tena.

MAPUMZIKO:
Dk 40, Yanga wanafanya shambulizi kali lakini Ruvu Shooting wanaonyesha ustadi mkubwa na kuokoa.

Dk 16, Msuva anainua mpira vizuri lakini kipa Benjamin Haule anauona na kuokoa kwa ustadi mkubwa.

Dk 13, Nizar anapiga shuti kali na linapita sentimeta chache pembeni, ilikuwa baada ya kupokea pasi ya chuji.

Dk 10, Aidan nusura aifungie Shooting lakini Barthez anaonyesha umahiri na kuokoa.

YANGA: Barthez, Juma Abdul, Oscar Joshua, Twitte, Cannavaro, Chuji, Msuva, Domayo, Kiiza, Niizar na Niyonzima.


RUVU; Benjamin Haule, Michael Aidan, Mau Bofu, brahim Shaaban, Mangasini Mangasini, Gideon Tepo, Ayoub Kitale, Ernest Ernest, Hassan Dilunga, Said Dilunga na Abrahman Mussa.


 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic