March 16, 2013




Kama utani vile, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Man City wameuwawa kwa kuchapwa mabao 2-0 na wenyeji wao Everton.

Everton waliokuwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Goodson Park jijini Liverpool, wamefanikiwa kushinda na hadi sasa wanaendelea kushangilia na ushindi licha ya kucheza kwa zaidi ya dakika 25 wakiwa pungufu.

Walibaki 10 uwanjani baada ya Pienaar kutolewa kwa kadi nyekundi ikiwa ni ya pili ya njano.

Osman alifunga bao la kwanza katika dk ya 32 kwa shuti kali takribani mita 30 na ushee. Linawezekana likawa moja ya mabao bora ya EPL msimu huu.


Pamoja na kuwa pungufu, Everton waliokuwa wanashangiliwa kwa nguvu na mashabiki wao, kipindi cha pili walipambana na dakika za majeruhi, Jelavic akamaliza mzizi wa fitina kwa kufunga bao la pili.

Wakati Everton walikuwa wakiendelea na sherehe, kocha Roberto Mancini na vijana wake walikuwa wakilaumu kuhusiana na mpira alioshika kiungo Fellaini ndani ya 18 katika dakika ya 89.

Kutokana na kipigo hicho, City wameipa nafasi Man United kuongeza pengo la kileleni hadi kufikia 15 huku zikiwa zimebaki mechi nane kumaliza msimu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic