1. Tegete akitishia kuondoka na pochi ya Mbogo...
Pamoja na kuwa katika harakati za
kufanyiwa upasuaji, beki Ladslaus Mbogo wa Yanga alionekana kuwa makini sana na
pochi yake ya kuhifadhia fedha.
2. Mbogo akisisitiza Tegete arudishe pochi yake chini ya himaya..
Mbogo maarufu kama Mnyama ambaye
amefanyiwa upasuaji wa shavu lilikokuwa na uvimbe, hata baada ya upasuaji huo,
alihakikisha pochi hiyo ikiwa pembeni chini ya uangalizi wake.
Hali hiyo ilisababisha awe katika
wakati mgumu baada ya wachezaji wa Yanga kumtembelea katika hospitali ya
Mwananyamala alipolazwa.
Mshambuliaji, Jerry Tegete ndiye
alikuwa akihoji kuhusiana na pochi hiyo, alimuuliza Mbogo mara kadhaa kama
anaweza akaondoka na pochi hiyo na kuihifadhi au aipeleke kwake.
Pamoja na kukumbushwa kwamba yuko
hospitali hivyo hatakuwa na matumizi ya fedha, lakini Mbogo akasisitiza lazima
abaki nayo.
Tegete amekuwa akitaniana sana na
Mbogo, hivi karibuni beki alichana kiatu cha Tegete baada ya ‘kumuachia’ daruga
wakati wakiwa mazoezini.
Mbogo anaendelea vizuri na Kocha
Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts alikwenda kumtembelea leo ili kumjulia hali.
3. Mbogo akikagua kama kweli Tegete ameweka pochi yake vizuri, Msuva anakufa na kicheko...
0 COMMENTS:
Post a Comment