March 17, 2013






TANZIA:
Uongozi wa klabu ya Yanga unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi Hamza Said al maarufu kama Zola au Chiluba, kifo kilichotokea leo alfajiri kwa ajali ya gari.

Zola amegongwa gari katika makutano ya mitaa ya Rufiji/Congo, Kariakoo jijini Dar es Salaam.


Marehemu Zola alikua mfanyakazi katika Sekretatriet wa klabu ya Yanga mpaka unamkuta umauti alfajiri ya leo.

Taratibu za mazishi zinapangwa kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu. Taarifa zinaeleza, mwili wa marehemu utapumzisha kesho saa 10 jioni kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar

Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen

BARAKA KIZUGUTO
MSEMAJI YANGA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic