March 16, 2013


Unakumbuka ile mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1984 wakati Bebeto alipoifungia bao dhidi ya Uholanzi?

Moja kwa moja akakimbilia kwenye kona ya uwanja na kuanza kushangilia akisaidiana na Romario na Mazinho kwa staili ya kubembeleza mtoto. 

Staili hiyo imekuwa maarufu sana, lakini siku hiyo Bebeto alikuwa anafurahia mkewe kujifungua mtoto wa kiume aitwaye Mattheus.

Sasa sikiliza, huo Mattheus anatakiwa na klabu ya Juventus baada ya kufanya vizuri na Flamengo ya Brazil, tayari amefikisha umri wa miaka 19.

Mattheus amekuwa aking’ara na Flamengo pamoja na timu ya taifa ya Brazil chini ya miaka 20.

Magwiji hao wa Italia, wako tayari kutoa pauni milioni 1.5 (zaidi ya Sh bilioni 3.9).
Taarifa zinaeleza ni kama vile dili limeshakamilika na mambo yakienda vizuri, siku chache kijana huyo atakuwa ametua Turin kuanza kazi na vigogo hao wa Italia.

Mattheus alianza kucheza timu ya wakubwa mwaka jana mwezi Februari na timu yake hiyo kutoka mji wa Rio ikatoka sare tasa na Olaria. Baba yake alikuwa jukwaani akishuhudia.

Bebeto mwenye miaka 49, sasa ameamua kuwa mwanasiasa, hivi karibuni aliteuliwa kuwa mmoja wa wanasiasa waliofanya vizuri katika chama cha Democratic Labour.
Bebeto alikuwa maarufu uwanjani wakati huo akishirikiana na Romario na Brazil ilifanikiwa kutwaa kombe mwaka huo nchini Marekani huku wao wakiwa gumzo.
Mattheus, kulia akiwa na rafiki yake...

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic