Pamoja
na kumchezesha kiungo mshambuliaji wake wa zamani wa Simba, Uganda ilishindwa
kufua dafu dhidi ya wenyeji wake Liberia.
Liberia
imeonyesha si timu ya mchezo baada ya kuichapa The Cranes kwa mabao mawili
katika mechi iliyochezwa jana kuwania kucheza fainali ya Kombe la Dunia nchini
Brazil.
Okwi
ambaye sasa anakipiga katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia, alishindwa
kuonyesha cheche zake na wenyeji wakafanikiwa kushinda.
Kocha
Bobby Williamson aliamua kumtoa Okwi katika dakikia ya 70 na nafasi yake
ikachukuliwa na Roberto Ssentongo ambaye pia aliwahi kukipiga Simba.
Pamoja
na mabadiliko pia ya kumtoa Mosses Oloya na Patrick Kizzito na nafasi zao
kuchukuliwa na Boban Zirintusa na Said Kyeyune, Uganda haikuweza kubadilisha
kitu.
Liberia
ilipata bao kila kipindi la kwanza likifungwa na Patrick Wleh katika dakika ya
36 na Anthony Laffor akafunga la pili katika dakika ya 50.
0 COMMENTS:
Post a Comment