March 21, 2013

Manji akiwa na Ridhwani...
 
KAMATI ya Utendaji ya Yanga imemteua Ridhiwani Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa jengo la klabu hiyo la Mafia, lililopo Mtaa wa Livingstone, Kariakoo jijni Dar es Salaam.

Akimtangaza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji alisema wameamua kumteua Ridhiwani kwa kuwa ni mwanasheria, hivyo wanaamini atawasaidia katika mambo ya kisheria.

Ridhwani na Manji...

Baada ya uteuzi huo, Ridhiwani sasa anatarajiwa kuteua kamati yake ambayo inatarajiwa kuundwa na watu wenye taaluma mbalimbali, wakiwemo wahandisi.

“Tumeshawapa notisi wapangaji wa jengo hilo ili watupishe tuanze ukarabati haraka iwezekanavyo. Tunataka tuwe na jengo la kisasa ambalo litakuwa na manufaa kwa klabu kwa kuhakikisha linakuza uchumi wa timu,” alisema Manji.

Akizungumza baada ya uteuzi huo, Ridhiwani aliishukuru kamati ya utendaji kwa kumpa wadhifa huo na kuahidi kutumia akili na nguvu zake zote ili jengo hilo limalizike likiwa katika ubora wa hali ya juu.


Manji na Katibu Mkuu Yanga, Lawrance Mwalusako...

 “Naahidi kujenga ghorofa kubwa lenye hadhi, nitahakikisha nateua wajumbe wenye uelewa mkubwa nitakaosaidiana nao,” alisema Ridhiwani.

Katika hatua nyingine, uongozi wa Yanga umeamua kusitisha kwa muda ujenzi wa Uwanja wa Kaunda, kwa kuwa umetuma barua serikalini tangu Februari, mwaka huu kwa ajili ya kupata ruhusa juu ya uwanja huo kuambatana na hoteli kubwa pamoja na majengo mengine ya biashara lakini hawajajibiwa.

Wilbert Molandi na Joan Lema (CHAMPIONI)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic