Niko
Mwanza, nyumbani kwetu nimerejea huku kutokana na matatizo ya kifamilia.
Pamoja na
mambo mengine, leo asubuhi nimekuwa na furaha sana baada ya Mzee wangu, Patrick
Yondani alipoamua kunitembelea.
Patrick
Yondani ndiye baba mzazi wa beki nyota wa Yanga, Kelvin Yondani. Leo alikuja
kunitembelea na kunijulia hali. Kelvin ana bahati ya kupata baba kama huyu, niamini 'he's very understanding'.
Yondani ni kati ya wachezaji wa zamani wa soka, yeye alikuwa mshambuliaji tofauti na mwanaye ambaye ni tegemo la safu za ulinzi za Yanga na Taifa Stars.
Baadaye
tulibadilisana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya soka, mzee anajua
mambo mengi sana ya soka, ufahamu wake uko juu.
Nikatamani
siku moja angepata nafasi ya uongozi, tulizungumza mambo mengi kuhusiana na
soka kwa ujumla, ikiwemo kuhusiana na Toto African, timu ya hapa Mwanza ambayo
inapigania ‘roho’ yake ili isitelemke daraja.
Nashukuru
sana mzee kwa kuonyesha kijana wako pamoja na kwamba una majukumu kibao hapa
jijini Mwanza.
PICHA ZOTE NA WIFE
0 COMMENTS:
Post a Comment