Viongozi wa Simba wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kukanusha
mambo mengi, lakini hali halisi iko hivi, mshambuliaji wake, Felix Mumba Sunzu
ameondoka nchini kimyakimya.
Sunzu ameondoka bila ya kumuaga mtu yoyote, tena inaelezwa
akiwa amepewa fdha ya kukata tiketike ya ndege kwenda kwao Zambia na kiongozi
mmoja wa zamani wa Simba.
“Kweli Sunzu hayupo nchini, ameondoka zake na aliyempa fedha
ya nauli tunamjua,” alisema mmoja we viongozi walio katika kamati za wa Simba.
“Unajua kuna kitu kimoja, kuna watu wanataka Simba ionekane
imefeli baada ya wao kuondoka. Kweli wanatuumiza sana.
“Sasa Sunzu ameondoka lakini tunasikia kuna hujuma inaendelea
kufanywa ili wachezaji waendelee kutuumiza. Si kitu chake.”
Inaelezwa, Sunzu ambaye alikuwa mchezaji analipwa mshahara
mkubwa kuliko mwingine yoyote nchini, ameondoka mkataba wake ukiwa umebakiza
mwezi mmoja tu.
Sunzu alikuwa analipwa dola 3,500 kwa mwezi, hivyo kuwa
mchezaji ghali zaidi kuliko wote kwa maana ya mshahara katika Ligi Kuu Tanzania
Bara.
Maana yake, hatarejea tena Simba, ingawa ilielezwa kulikuwa
na juhudi zinafanywa kuhakikisha anarejea nchini kumalizia mechi zilizobaki
ambazo zinaweza kuikoa Simba hadi kushika nafasi ya pili.
Hii ni mara ya pili kwa Sunzu kuondoka nchini. Miezi miwili
iliyopita alirejea kwao Zambia, baadaye akaja nchini na baba yake mzazi ambaye
aliomba kuvunja mkataba kwa madai mwanaye ni mgonjwa.
Simba waliafiki wakitaka kama atauzwa, basi nao walipwe. Lakini
siku chache baada ya kurejea Zambia, alirejea nchini na kujiunga tena na Simba
na ikaelezwa alikosa timu ya kucheza ndiyo maana akaamua kurudi tena Msimbazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment