Kikosi cha Simba kinachoundwa na vijana wengi, leo
kimefanya mauaji katika mechi ya kirafiki dhidi ya Singida United kwenye Uwanja
wa Namfua mjini Singida kwa kuichapa kwa mabao 4-0.
Singida ndiyo mji anaotokea mlezi wa Simba, Rahma
Al Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki.
Simba ambayo iko njiani kwenda mjini Bukoba kuwavaa
Kagera Sugar, Jumatano ijayo, ilionyesha soka safi na la kuvutia.
Kikosi hicho kiliundwa na vijana wengi zaidi, huku
wakongwe kwa asilimia 98 wakiwa benchi na vijana wakaonyesha kuwa kazi
wanaiweza.
Kikosi kilichopangwa na Patrick Liewig kutoka
Ufaransa, kilikuwa kinasomeka hivi Abuu Hashim, Haruna Shamte, Waziri Omar,
Hassan Hassan, Hassan Khatib, Jonas Mkude, William Lucian /Said Mangela, Mselem
Salum, Christopher Edward, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Marcel Kahezya ‘Rivaldo’
/Haroun Chanongo.
wauaji wa mabao hayo manne walikuwa ni Rama Kipalamoto aliyefunga kiufundi kwa mguu wa kulia, Mselemu Salum, Omar Waziri na Singano ‘Messi’.
Simba iko katika kampeni kubwa ya
kupambana na wachezaji wakongwe ambao wamekuwa wakionekana ni tatizo kubwa hasa
katika nidhamu na kuamua kuwaamini vijana.
Ingawa mashabiki wamekuwa wana hofu
kutokana na kukosekana kwa majina makubwa katika kikosi hicho, lakini vijana
hao wamekuwa wakiendelea kufanya vizuri.
Mchezo dhidi
ya Kagera Sugar unaonekana kuwa muhimu zaidi na mgumu kwa Simba kutokana na
uimara wa timu hiyo inayonolewa na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Abdallah ‘King
Mputa’ Kibadeni.
0 COMMENTS:
Post a Comment