Wiki moja
tu baada ya kumaliza adhabu ya miezi sita ya kuzuiwa kuendesha gari, Rio
Ferdinand amekutana na adhabu nyingine ya kulipa faini ya pauni 200 (zaidi ya
Sh 520,000).
Beki huyo
wa Man United ambaye amekulia katika kitongoji cha watukutu cha Peckham
alikamatwa kwenye moja ya mitaa ya jijini la Manchester akiwa ‘kiatu’ kiana.
Rio
hakuwa katika kasi kubwa akiwa na gari lake aina ya Jaguar XJ Supersport V8.
Ilikuwa kama saa 2.41usiku wakati akiwa katika eneo linalotakiwa kutembea spidi
40 tu, yeye akazidisha hadi 48.
Baada ya
kuonyeshwa spidi alizozidisha hakuwa na ujanja tena, pamoja na kuomba msamaha lakini
ilishindikana na sheria ikachukua mkondo wake, akapigwa faini hiyo.
Beki huyo
amekuwa akituhumiwa kutokana na mikasa isiyoisha ikiwemo ya uwanjani na nje,
lakini mwenyewe amekuwa akisisitiza anataka kuishi maisha yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment