Timu
ya soka ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mechi
ya awali kuwania kucheza Kombe la Dunia.
Stars
imefanikiwa kuibuka na ushindi huo mnono baada ya kuwachapa Morocco katika
mechi iliyochezwa kwenye Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao
ya Stars yamefungwa na Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta, wote wawili ni
washambuliaji wa TP Mazembe ya DR Congo.
Pamoja
na kuifunga Morocco, kikosi cha Stars chini ya Kocha Kim Poulsen kilitawala
mchezo kwa muda mwingi na mashabiki walionyesha uzalendo kwa kuwashangilia
mwanzo mwisho.
Stars
iko katika kundi moja na Ivory Coast, Gambia na Morocco na ushindi huo
umewafanya wakae kileleni mwa kundi hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment