Kiungo nyota
wa PSG ya Ufaransa, David Beckham ametoa mpya ya mwaka baada ya kula ‘bonge’ ya
mweleka wakati akipiga faulo.
Beckham
raia wa England alianguka wakati akionyesha utaalamu wa kupiga mipira ‘iliyokufa’
kwa wachezaji vijana nchini China ambako ana ziara ya kibalozi ya siku tano.
Akiwa ndani
ya vazi safi kama mtu anayekwenda ofisini, Beckham alijisahau kwamba hakuwa na ‘njumu’
hivyo kuachia shuti kali nay eye akateleza hadi chini.
Hata hivyo
vijana wa timu ya Zall Club walionyesha kutojali hilo la kuanguka kwa Beckham
badala yake walifuatilia mpira ulipokuwa umetua.
Yeye
Beckham aliinuka mara moja huku akicheka na akaendelea na ratiba zake kama
zilivyokuwa zimepangwa.
Ziara ya
Beckham nchini humo imekuwa gumzo kwa kuwa amepokelewa kwa makeke na imeonyesha
kwamba kweli ni mtu anayekubalika kwa kiasi kikubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment