April 10, 2013



Baada ya upasuaji mkubwa uliofanyika kwa mafanikio makubwa, beki wa Yanga, Mbogo Ladislaus, atafanyiwa upasuaji mwingine.

Mbogo alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Mwananyama kuondoa uvimbe katika shavu lake.

Lakini amepangiwa kufanyiwa upasuaji mwingine katika shavu lake kwa lengo la kuondoa ngozi ambayo ilitokana na upasuaji we awali.


“Kweli daktari wa timu (Yanga), ameniambia kuna upasuaji unatakiwa kufanyika. Lengo ni kurekebisha mambo yaende vizuri na mimi sina tatizo,”  alisema Mbogo, baba wa watoto wawili.

Kuhusiana na hilo, daktari wa Yanga, Nassor Matuzya alisema upasuaji wa pili utasaidia kurudisha muonekano mzuri kwa Mbogo.

 “Awali tulifanya zoezi la kuondoa nyama iliyokuwa imevimba, kulikuwa na mafanikio makubwa, sasa kidonda kinakaribia kupona na baada ya hapo tutafanya upasuaji mwingine kurudisha ngozi yake.

“Lazima ngozi ya eneo hilo itakuwa imetanuka kwa kuwa ilikuwa na kitu ndani, baada ya upasuaji wa pili tunaamini mambo yatakaa vizuri,” alisema Matuzya.

Mbogo alilazimika kumhamishia mkewe Jema jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata huduma nzuri. Awali mkewe alikuwa akiishi jijini Mwanza ambao ni mji aliozaliwa na kukulia kisoka beki huyo wa zamani wa Toto African.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic