April 7, 2013



Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameipinga kauli ya  Kocha Mkuu wa Toto, John Tegete kwamba alipigwa na shabiki.

Julio amesema yeye ndiye aliyepigwa na alimuona kiungo Emmanuel Swita wa Toto African akifanya shambulizi hilo.
“Tokea awali nilieleza, kulikuwa na hali ya kuteteana na Tegete ingawa tunaheshimiana lakini alionyesha si muungwana na kumtetea mchezaji wake.

“Tokea ninautafuta mpira wetu, yeye alikuwa anatetea akishirikiana nadaktari wa timu. Nashukuru sana, lakini mimi ndiye niliyepigwa na niliona aliyenipiga,” alisema Julio.

Hivi karibuni, Tegete ambaye ni baba mzazi wa mshambuliaji Jerry Tegete wa Yanga alisema Julio alipigwa ngumi na shabiki wa Toto na si Swita kama alivyosema yeye.

Tafrani hilo lilitokea mara baada ya mchezo kati ya Toto na Simba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Julio alisema, alipigiwa simu na mdau aliyekuwa jukwaani akimueleza Swita aliiba mpira mmoja wa Simba na kuingia nao kwenye gari, Julio akaamua kuzima basi lililokuwa limewabeba wachezaji wa Toto ili mpira huo utafutwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic