April 7, 2013





Kipa nyota wa zamani wa Arsenal, David Seaman amezidi kutia chumvi kidonda cha Kocha Arsene Wenger kwa kusema alikosea kumuuza Robin van Persie kwa Man United.

Seaman ambaye alikuwa kipa mahiri wa Arsenal chini ya Wenger alisema hajachoka kushangaa kila anapomuona van Persie akiwa katika jezi ya Man United.


Tokea amejiunga na Man United akitokea Arsenal, katika mashindano yote, van Persie tayari amefunga mabao 23 katika mechi zote akiwa na timu hiyo chini ya Alex Ferguson.

Seaman alisema: ”Wakati mwingine kunakuwa na ugumu sana kuuza mchezaji ambaye anategemewa, tena ugumu unaongezeka kama anayeuzwa ni nahodha, huwa inaisumbua timu.

“Inawezekana ni msukumo wa kibiashara, lakini bado ni si sahihi kumuuza nahodha tena kwa Manchester United. Utaona hapo zamani mambo haya hayakufanyika na biashara ziliendelea.

“Hauwezi kusikia Arsenal wanamuuza mchezaji kwenda Manchester na sisi tulikuwa na wachezaji wengi tu.”

Pamoja na kwamba Arsenal imeanza kurejea katika msitari kwa kushinda mfululizo hadi kufikia nafasi ya nne katika msimamo wa Premiership, lakini bado inaonekana imekuwa si timu ya uhakika na mashabiki wamekuwa wakimlalamikia Wenger ikiwa ni pamoja na suala la kumuuza van Persie.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic