April 9, 2013



 Man City wamethibitisha alichokisema Kocha wao Roberto Mancini kwamba Man United wanafungika ila wanaokutana nao wamekuwa wakiwahofia tu.



Mechi hiyo ya watani iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka, imemalizika kwa City wakiwa ugenini kushinda kwa mabao 2-1. 

Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Old Trafford ilikuwa ya ushindani mkubwa kuanzia mwanzo.

City ndiyo walitangulia kupata bao kupitia Milner ambaye aliachia mkwaju mkali wa chinichini katika dakika ya 51, ukajaa wavuni wavuni.

Lakini United wakasawazisha katika dakika ya 59 baada ya mpira wa faulo wa van Persie na Jones kuugonga kumgonga Vincent Kompany na kujaa wavuni.

Wakati ikionekana kama mechi hiyo itaisha kwa sare ya bao 1-1, Kun Aguero aliyeingia kuchukua nafasi ya Samir Nasri, akaonyesha ana uwezo binafsi baada ya kuwatoka wachezaji watatu na kupachika bao la pili katika dakika ya 79.

Baada ya hapo, mpira ulionekana kuchafuka na ubabe kutawala huku wachezaji wa Man United wakionekana kujaa jazba.
Kutokana na ushindi huo, City wamefikisha pointi 66 na kuzidi kujishindilia katika nafasi ya pili na United wanabaki kileleni na pointi 78.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic