April 8, 2013




Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtaka mshambuliaji Nsa Job wa Coastal Union kuwasilisha maelezo yake juu ya madai kuwa alipewa rushwa ya Sh milioni mbili ili asiifunge moja ya timu vigogo vya soka nchini.

Hilo ni balaa lingine kwa Nsa katika msimu huu baada ya kulazimika kukosa mzunguko wote wa pili kutokana na kuumia vibaya katika mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza dhidi ya JKT Ruvu.


Hivi karibuni, Nsa aliingia katika mgogoro mkubwa na viongozi wa Coastal baada ya kueleza hakukuwa na aliyekwenda kumpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati ajarejea kutoka India kwenye matibabu.



Job alikaririwa Aprili 3 mwaka huu na kituo cha redio cha Clouds FM katika kipindi cha Amplifier kuwa alipewa kiasi hicho cha fedha na kiongozi wa timu husika ili asiifunge katika mechi ya Ligi Kuu ya Bara, lakini alipokea fedha hizo na kuifunga timu hiyo.

Baadaye kiongozi huyo alikuwa akimtaka arejeshe fedha hizo. Pia TFF imekiandikia kituo hicho cha redio kutaka nakala ya kipindi hicho ili pamoja na maelezo ya mshambuliaji huyo vipelekwe katika Kamati ya Nidhamu kwa ajili ya hatua za kinidhamu.

TFF itachukua hatua kali dhidi ya Job iwapo hatawasilisha maelezo yake kuhusiana na suala hilo, na imetaka wadau kutoa ushirikiano ili iweze kupambana kikamilifu na vitendo vya rushwa kwenye mpira wa miguu.

 Uchunguzi wa Salehjembe umeonyesha msimu huu Nsa alicheza mzunguko wa kwanza tu na kuumia katika mechi ya mwisho.

Kama ni timu tatu kubwa yaani Yanga, Simba na Azam FC hakuna aliyeifunga ingawa alicheza katika mechi zote tatu.

Alianza katika mechi dhidi ya Simba mjini Tanga, matokeo yalikuwa ni sare ya bila kufungana na Novemba Mosi Azam FC na kukutana na kipigo cha mabao 4-1 moja kule Chamazi Complex, bao pekee la Coastal likiwa limefungwa na Jerry Santo.

Mechi ya mwisho ya timu kubwa ilikuwa dhidi ya Yanga, Novemba 11 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na wageni Coastal Unioni wakalambishwa mabao 2-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic