Mtanzania Mbwana Samatta ameendeleza mguu wa mabao baada ya kupiga moja wakati timu yake ya TP Mazembe ilipoinyoa Muchudi ya Botswana mjini Lubumbashi kwa mabao 6-0.
Maana yake Mazembe ifuzu kwa jumla ya mabao 7-0 baada ya kushinda ugenini mjini Gaborrone kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Samatta.
Kwa ushindi huo sasa Mazembe itakutana na wababe wa Afrika Kusini, Orland Pirates ya Soweto.
Timu hiyo kutoka katika kitongoji hicho maarufu zaidi nchini Afrika Kusini, ndiyo inayoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi zaidi nchini humo.
Katika mechi ya jana, nahodha Tresor Mputu alifunga mabao mawili hivyo kuifanya Mazembe iweke rekodi mpya.
Mazembe imeweka rekodi ya kuwa moja ya timu zilizofanya vizuri zaidi tokea Shirikisho la Soka Afrika (Caf) lianze kutumia mfumo wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1997 badala ya ule wa Klabu Bingwa Afrika uliokuwa ukitumika.
Tokea mwaka 1997 ilipoanza Ligi ya Mabingwa Afrika, Mazembe imeingia mara nane katika hatua ya 16 bora kama ilivyofanya safari baada ya kuinyoa Mochudi.
Wachezaji wa Mazembe ambao wamecheza michuano hiyo mara nyingi zaidi ni ni Mputu, Patou Kabangu na mshambuliaji Mzambia, Given Singuluma.
MATOKEO MENGINE YA LIGI YA MABINGWA...
EST
|
1-0
|
Primeiro de Agosto
|
Orlando Pirates
|
2-1
|
Zanaco
|
Entente Setif
|
4 - 2
|
ASFA Yennega
|
Al Merreikh
|
1-2
|
Recreativo de Libolo
|
Al Hilal
|
3 - 1
|
Sewe San Pedro
|
Stade Malien
|
2-0
|
Casa Sport
|
AC Leopards
|
Vs
|
Kano Pillars
|
AS Vita Club
|
0 - 0
|
Zamalek
|
Rangers
|
2-0
|
Vital'O
|
Coton Sport
|
2-1
|
AF Amadou Diallo
|
Asante Kotoko
|
1-1
|
JSM Bejaïa
|
Union Douala
|
1-0
|
FUS
|
Djoliba AC
|
1-1
|
Saint George
|
Dynamos
|
1-0
|
C.A.B
|
Al Ahly
|
2-0
|
Tusker
|
TP Mazembe
|
6-0
|
Mochudi C.Chiefs
|
0 COMMENTS:
Post a Comment