April 8, 2013



Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa), limemtimua kocha wa timu ya taifa The Cranes, Bobby Williamson.

Katika kikosi cha The Cranes kilichochapwa na Liberia, Williamson alimpa nafasi ya kucheza dakika 70 mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye sasa anakipiga katika timu ya Etoile du Sahel.

Williamson ametimuliwa baada ya The Cranes kuchapwa kwa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Liberia mjini Monrovia katika mechi ya awali kuwania kucheza Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.


Uganda imechukua uamuzi kwa kocha huyo ambaye alionekana na mafanikio makubwa kwa kutwaa Kombe la Chalenji mara nne.

Kocha huyo raia wa Scotland alianza kuifundisha The Cranes mwaka 2008 na taarifa zimeeleza kuwa uamuzi huo umelenga kuleta mabadiliko katika benchi la ufundi.

Uganda ina pointi mbili tu baada ya kucheza mechi tatu katika mechi hizo za kwuania kucheza Kombe la Dunia 2014.

Mechi zilizobaki ambazo zitatoa majibu ya kama watasonga hatua inayofuatia zitakuwa Juni wakiwa nyumbani ni dhidi ya Liberia na  Angola. 

Ugandanusura ifuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika lililofanyika nchini Afrika Kusini lakini mikwaju ya penalti ikawang’oa na Zambia wakafuzu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic