April 7, 2013

Beki wa pembeni wa Barcelona, Eric Abidal amemshukuru hadharani binamu yake aliyejitolea kumpa figo yake.

Abdal raia wa Ufaransa alirejea wakati Barcelona ikipambana na Real Mallorca kuchukua nafai ya Gerard Pigue. Barca ilishinda mabao 5-0, huku Cesc Fabregas akipiga hat trick yake ya kwanza.

Mashabiki wa Barcelona walionyesha upendo mkubwa kwa beki huyo mwenye miaka 33 na kusimama wakionyesha walikuwa wakimkaribisha tena nyumbani.


Siku chache zilizopita, Abidal alipita katika vipimo kuonyesha yuko fiti na anaweza kujiunga na wenzake baada ya kipindi kirefu cha matubabu.
Hata baada ya mechi hiyo, Abidal alionyesha fulana yake iliyokuwa na maneno “Merci mon cousin”, akionyesha kumshukuru binamu yake huyo aliyempa figo baada ya kwake kuonekana ina matatizo.

“Namshukuru sana binamu yangu, hakika bila ya yeye mimi nisingekuwa hapa leo,” alisema Abidal akionyesha kuwa ni mwenye furaha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic