April 13, 2013



 Kikundi cha vijana wa Kipalestina ambacho hujihusisha na masuala ya haki ya Wapalestina, kimechukua jukumu la kuchoma moto jezi za Barcelona.

Pamoja na kuchoma moto jezi hizo, memba wa kundi hilo, tokea juzi wamekuwa wakizunguka maeneo mbalimbali kueneza chuki dhidi ya timu hiyo ya Hispania yenye mashabiki lukuki.

Hatua hiyo ya kikundi hicho imetokana na taarifa kuwa Barcelona, imefikia makubaliano ya kucheza mechi za kirafiki jijini Tel Aviv wakati wa majira ya joto.

Kitendo hicho kimeonyesha kuwaudhi memba wa kikundi hicho kwa kuwa wanaamini kufanya hivyo ni sawa na Barcelona kuwaunga mkono Waisrael na kutaka waishi kwa raha mustarehe huku wakiendeleza matatizo kwa Wapaletsina.

Bado uongozi wa Barcelona haujazungumza lolote kuhusiana na tukio hilo ambalo taarifa zake zimeshatua jijini Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic