Shirikisho
la Soka Afrika (Caf) limeteua waamuzi kutoka Shelisheli kuchezesha
mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam na AS FAR
ya Morocco itakayofanyika Aprili 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi
hao ni Emile Fred atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Steve Maire na Jean
Ernesta. Mwamuzi wa mezani (fourth official) atakuwa Jean Claude Labrossa.
Kamishna wa mechi hiyo ni Abbas Sendyowa kutoka Uganda.
Wakati
huo huo, CAF imemteua Mtanzania Alfred Lwiza kuwa Kamishna wa mechi ya kwanza
ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati ya Liga Muculmana ya Msumbiji na
Wydad Casablanca ya Morocco.
Mechi
hiyo itakayochezwa kati ya Aprili 19,20 au 21 mwaka huu nchini Msumbiji
itachezeshwa na waamuzi kutoka Zimbabwe wakiongozwa na Ruzive Ruzive.
BONIFACE WAMBURA
MSEMAJI TFF
0 COMMENTS:
Post a Comment