Mshambuliaji Sergio Aguero amesaini mkataba mpya na
klabu yake ya Manchester City ambao
utamalizika mwaka 2017.
Fowadi huyo mkali alikuwa akiwaniwa na Real Madrid
lakini Man City wameamua kuzima kila kitu kwa kumsajili ili aendelee kubali
Etihad.
Imeelezwa kocha mpya wa Man City, Manuel Pellegrini
ndiye ameongoza chachu ya kutaka Muargentina huyo aongezewe mkataba.
“Nasikia furaha kubwa kuongeza mkataba mpya,”
alisema Aguero.
Msimu uliopita, alifunga bao muhimu dakika za
mwisho katika mechi dhidi ya QPR na kuipa City ubingwa iliokuwa inautafuta kwa
kipindi kirefu.
0 COMMENTS:
Post a Comment