Pepe akiwa na Rais wa Madrid, Florentino Perez |
Uongozi wa Real Madrid umetangaza kwamba hautamuuza
beki wake wa kati Pepe.
Tayari klabu kadhaa zilijitokeza kutaka kumyakua
beki huyo mtukutu baada ya kutocheza mechi nyingi za mwishoni mwa msimu ikionekana
ilikuwa adhabu kwake.
Pepe alikumbana na adhabu hiyo ya kimyakimya kutoka
kwa Jose Mourinho baada ya kutoa kauli ya kumtetea kipa Iker Casillas aliyekuwa
na ugomvi na Mourinho.
Kupitia mtandao wake, Madrid imesema haiwezi
kumuuza Pepe kwa kuwa anaendelea kutegemewa kuimarisha ulinzi.
“Pepe ameishataarifiwa na uongozi wa juu kwamba
hatauzwa, hivyo hilo lieleweke kwamba ataendelea kubaki Madrid kwa msimu mmoja
mwingine,” ilieleza sehemu hiyo ya taarifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment