Neyma na baba yake ambaye pia ni wakala wake... |
Baba wa mshambuliaji nyota wa Santos, Neymar ambaye pia ndiye wakala wake amekiri kukutana na uongozi wa Barcelona na kufanya mazungumzo.
Neymar Da Silva alisema pamoja na kukutana na Barcelona lakini wapianzani wao Real Madrid pia wamekuwa wakiwania saini ya mshambuliaji huyo nyota wa Brazil.
Neymar&Messi |
Da Silva aliliambia gazeti la Lance la Brazil kwamba dau la mshambuliaji huyo hadi sasa ni euro milioni 60.
“Nimezungumza na klabu zote hizo kubwa za Hispania lakini bado hatujafikia mwafaka na upande wowote, hivyo Neymar anaendelea kubaki kuwa mchezaji halali wa Santos,” alisema.
Inaelezwa Da Silva Lance alikutana na Mkurugenzi wa Soka wa Barcelona, Raúl Sanllehí aliyefunga safari hadi Brazil na kufanya naye mazungumzo juzi Alhamisi.
Blogu hii ililipoti juzi kwamba Barcelona walikuwa wamempeleka mkurugenzi huyo nchini Brazil ili kuanza mchakato wa kumnasa Neymar ambaye ataongeza makali kwa kushirikiana na Lionel Messi.
0 COMMENTS:
Post a Comment