Sure Boy akithibiti mpira mbele ya kiungo wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi |
Kocha Mkuu
wa Azam FC, Stewart John Hall ameamua kumuacha nje kiungo wake nyota, Salum
Abubakari ‘Sure Boy’ kabla ya mechi ya leo ya kufunga msimu dhidi ya JKT
Oljoro.
Mechi hiyo
inapigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha na Sure atakuwa nje
ya kikosi.
“Nimefanya
hivyo kama sehemu ya kumpumzisha, amecheza mechi nyingi sana kwa msimu.
“Halafu
baada tu ya mechi atalazimika kuingia kambi timu ya taifa, hivyo nimeamuacha
Dar es Salaam ili aendelee na mapumziko,” alisema Hall raia wa Uingereza.
Kabla
ya hapo, Hall aliamua kuwaruhusu wachezaji wake wote wa kigeni kurejea makwao
na kutaka mechi yao leo ya kufunga msimu wacheze wazawa hasa wale ambao
hawakuwa wakipata nafasi mara kwa mara kwa msimu wote.
Azam
FC imemaliza msimu ikiwa katika nafasi ya pili kama ilivyokuwa msimu uliopita
na kujihakikishia nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa mwakani.
0 COMMENTS:
Post a Comment