Uongozi wa
Yanga, uko katika mchakato wa kuhakikisha wake, wapenzi na watoto wa wachezaji
wanakuwa uwanjani leo kushangilia pamoja kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Yanga imeamua
kutumia utaratibu huo ikiwa ni sehemu ya kufuata kama ambavyo timu nyingi za
Ulaya hufanya.
“Mawasiliano
yameishafanyika na sasa tuko katika hatua za mwisho kukamilisha kuhusiana na
wake, watoto na wapenzi wa wachezaji kuwa pale uwanjani.
“Tumeamua
kufanya hivi kama sehemu ya utaratibu kwa kuwa mambo yanabadilika duniani kote,
umeona namna mambo yanavyokwenda kila sehemu.
“Hivyo ni
vizuri kuiga vitu vizuri na ndiyo maendeleo yenyewe, tunaamini wengine
watatuiga sisi wakati mwingine,” kilieleza chanzo kutoka ndani ya Yanga.
Kama watafanya
hivyo leo, Yanga itakuwa timu ya kwanza kutumia utaratibu huo hapa Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment