Na Boniface Wambura, Addis Ababa
Balozi
wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa Stars
kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia
zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Ametoa
changamoto hiyo wakati alipotembelea mazoezi ya timu hiyo jana (Mei 29 mwaka
huu). Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi
nchini Ethiopia na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Addis Ababa.
“Watanzania
tunafurahi kutokana na uwezo mnaouonyesha, hasa baada ya kuifunga Morocco mabao
3-1. Kama mliwafunga nyumbani hata kwao mnaweza kuwafunga. Tunataka kuwaona
Maracana (Brazil) mwakani, mimi tayari ninayo tiketi mtanikuta kule,” amesema
Balozi Biswaro ambaye enzi zake aliwahi kuichezea timu ya Yanga.
Taifa
Stars ambayo iko Addis Ababa tangu Jumatatu (Mei 27 mwaka huu) imeweka kambi
katika hoteli ya Hilton ambapo Jumapili (Juni 2 mwaka huu) itacheza mechi ya
kirafiki na Sudan (Nile Crocodile) kwenye Uwanja wa Addis Ababa.
Balozi
Biswaro ameikaribisha Taifa Stars ubalozini Addis Ababa mara baada ya mechi
dhidi ya Sudan ambapo itakutana na baadhi ya Watanzania wanaoishi Ethiopia
kabla ya kuondoka alfajiri kwenda Marrakech, Morocco kwa kupitia Cairo, Misri.
Kocha
Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na kitaimarika
zaidi baada ya wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya
TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kujiunga nacho Juni 3 mwaka
huu jijini Marrakech kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8
mwaka huu.
Wachezaji
walioko katika kikosi cha Stars jijini Addis Ababa ni Juma Kaseja, Aggrey
Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto
Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis
Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas,
Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment