Kiungo nyota Mwingereza, David Beckham ametangaza kustaafu soka la
ushindani.
Beckham amewashitua wengi kutokana na uamuzi wake huo wa ghafla huku
akiwaacha midomo wazi PSG ambao walikuwa wamemuongezea mkataba wa mwaka mmoja.
Mwingereza huyo mwenye miaka 38, ametangaza
kustaafu na kusema amefikia ndoto ya kila alichokitaka na sasa ni wakati wa
kupumzika.
Akiwa na timu ya taifa ya England aliyowahi kuwa
nahodha, Bekcham aliichezea mechi 115 na kuwa mmoja wa wachezaji waliocheza
mechi nyingi wakiwa na timu ya taifa.
Hivi karibuni alitoa msaada mkubwa kwa PSG
iliyofanikiwa kutwaa ubingwa wa Ufaransa baada ya kukaa ‘kapa’ bila kitu kwa
miaka 19 iliyopita.
Beckham ndiye Mwingereza anayeshikilia rekodi ya
kutwaa makombe manne katika nchi tofauti baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu
England akiwa na Man United, Real Madrid (Hispania), LA Galaxy na PSG
(Ufaransa).
0 COMMENTS:
Post a Comment