Barcelona imepiga hatua katika uamuzi wake wa kutaka kumsaini
mshambuliaji nyota kutoka Santos ya Brazil, Neymar.
Catalan tayari wamemuagiza mkurugenzi wa soka wa timu yao, Raúl Sanllehí
ambaye hadi sasa yuko nchini Brazil kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu zaidi.
Pamoja na wapizania wao Real Madrid kuonyesha wanamtaka mchezaji huyo,
lakini Barcelona walishatanguliza euro milioni 10 mwaka 2011.
Wakati Rais wa Barcelona, milione Sandro Rosell alikutana na makamu wa
Rais wa Santos, Odilio Rodrigues Ijumaa iliyopita, lakini katika mkutano huo Raúl
Sanllehí alihudhuria pia.
Siku chache baadaye Rosell alilaumiwa kwa kutotokea katika mechi ya nusu
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mchezo wa kikapu kati ya Real Madrid na
Barcelona, lakini baadaye ikagundulika alikuwa katika mkutano huo muhimu wa
kuhakikisha anamnasa Neymar.
0 COMMENTS:
Post a Comment