May 30, 2013




Beki Godfrey Taifa atakuwa mchezaji wa kwanza kuachwa katika kikosi cha Yanga, imeelezwa.

Taita ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Villa Squad ya Kinondoni anaonekana kushindwa kumshawishi Kocha Ernie Brandts aliyemuweka kwenye watakaoachwa.

Pamoja na kushindwa kusmhawishi uwanjani, imeelezwa Taifa amekuwa mtukutu na aliwahi kufanya utovu wa nidhamu kambini mara mbili.

“Wakati mmoja aligombana na mchezaji mwenzake na kusababisha uharibifu katika hoteli ambayo walikuwa tumefikia,” kilieleza chanzo.
“hivyo kocha amemuweka katika kundi la wachezaji ambao lazima safari iwakute.”


Taita amekosa namba katika kikosi hicho, mfano namba mbili kuna Shadrack Nsajigwa ambaye pia namba hana uhakika, Juma Abdul na Mbuyu Twite ambao ndiyo wenye nafasi zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic