Uongozi
wa Yanga umesema umeelekeza nguvu zake katika kuanza ujenzi wa Uwanja wao wa
kisasa kwenye eneo la Kaunda jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji amesema wamekuwa wakiendelea na mchakato huo na mambo
yatakapokamilika, kazi ya ujenzi itaanza.
“Usione
tuko kimya, mchakato unaendelea nasi tunahitaji muda kwa ajili ya kujadili,
kujipanga na baadaye kuanza.
“Kamati
inayohusika na masuala hayo inaendelea tunakutana na wahusika na kujadili
halafu tunaangalia nini kinaendelea na nini tuendelee nacho.
“Hivyo
mnatakiwa kuvuta subira na baadaye mtaona mambo yanaendelea,” alisema Manji.
Tayari
uongozi Yanga ulishateua kamati inayoshughulikia suala hilo iliyo chini ya
Ridhwani Kikwete.
Lakini
kampuni inayohusika na ujenzi wa uwanja huo kutoka China, ilishakabidhi ramani
tatu kwa Yanga na wanatakiwa kuchagua moja ambayo itumike na ujenzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment