May 8, 2013




 Kiungo Michael Essien amewaalika wachezaji na kikosi kizima cha Real Madrid kwenda kucheza Ghana katika mechi maalum ya hisani itakayopigwa Juni 8 mjini Accra.

Essein ambaye amejiunga na Madrid akitokea Chelsea ya England, pamoja na kuwaalika wachezaji, pia ametoa mwaliko kwa kocha wa timu hiyo Jose Mourinho.

Mchezo huo ulioandaliwa na Essien na serikali ya Ghana umelenga kuhamasisha watu wenye shida lakini pia kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wenye matatizo.


Luka Modric na beki Ricardo Carvalho ambao wanaonekana kuwa karibu zaidi na Essien wamethibitisha kushiriki katika mechi hiyo ambayo itakuwa ya kukata na shoka kama kila kitu kitaenda vizuri.

Iwapo Madrid watakwenda, kwa Mourinho haitakuwa ni mara ya kwanza kwani aliwahi kusafiri hadi Ghana akiongozana na Essien kwa ajili ya kufanya shughuli za uchangishaji kuwasaidia watu wenye matatizo.

Mara ya kwanza, Essien aliandaa shughuli ya uchangishaji kusaidia watu wenye matatizo Mei, 2011 na ikawa na mafanikio makubwa na fedha zote zilizopatikana, Michael Essien Foundation ilizigawa kusaidia watu wenye matatizo.

“Watu wa Ghana wanapenda sana soka, kama kuna mechi ya soka utamuona kila mtu pamoja na wengine. Nimegawa kadi kwa wachezaji wote na imani yangu watakubali na mechi hiyo itafanyika,” alisema Essien.

Pamoja na wachezaji hao wa Real Madrid, wachezaji wengine ambao tayari wamemjibu Essien kwamba watakuwepo Accra kushirikiana naye ni Drogba, Adebayor, Kolo na Yaya Touré, Cissé, Malouda na Ferreira.

Lakini kuna wachezaji mahiri wa zamani pia wamekubali kujitokeza ambao ni Ginola, Weah, Makélélé, Ljungberg, Ballack  na Fabrice Muamba, mchezaji wa zamani wa Bolton ambaye alianguka ghafla uwanjani na kupoteza fahamu na baadaye akalazimika kustaafu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic