May 8, 2013



 
Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Premier League, Manchester United, wametangaza kwamba, Sir Alex Ferguson atastaafu kama meneja wa klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu. 

Sir Alex anatajwa kuwa ndiye meneja mwenye mafanikio makubwa katika historia ya soka la Uingereza.


Tangu alipojiunga na klabu hiyo mnamo mwaka 1986, ameshinda mataji mawili ya Klabu Bingwa Barani Ulaya, mataji kumi na tatu ya Ligi Kuu na Kombe la FA mara tano.


Katika taarifa yake, Sir Alex amesema ni muda muafaka kwake kustaafu wakati klabu ikiwa imejizatiti katika nafasi nzuri. Atabakia Manchester United kama mmoja wa wakurugenzi na balozi.

Tayari mashabiki mbalimbali wa soka hasa wale wa Man United wameonekana kuchanganyikiwa kuhusiana na suala hilo.

Maswali yanatawala kwa upande wa kocha gani atachukua nafasi yake, wengine wanaamini David Moyes wa Everton ndiye anapewa nafasi kubwa zaidi ya kuchukua nafasi hiyo.

Nafasi ya pili anapewa Jose Mourinho, hofu kubwa ni kwamba si kocha anayependa kutulia sehemu moja na Man United ingependa kuwa na kocha atakayekaa kwa kipindi kirefu.

Gumzo la Ferguson kujiuzulu linaonekana kuchukua nafasi kubwa ingawa wengi wanaona kama ni ndoto.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic