May 8, 2013




Simba imejihakikishia kushika nafasi ya tatu baada ya kufanikiwa kuifunga Mgambo Shooting kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mechi hiyo iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilipata bao pekee lililofungwa na Haruna Chanongo.

Ushindi huo, Simba imefanikiwa kufikisha pointi 45 ambazo zinaihakikishia kubaki katika nafasi hiyo kwa kuwa imebaki mchezo mmoja kama Kagera yenye pointi 40 na ina mchezo mmoja pia.


Maana yake hata kama Simba itapoteza dhidi ya Yanga, basi Simba itaendelea kubaki katika nafasi ya tatu.

Chanongo alifunga bao hilo baada ya kuwapangua mabeki wa Mgambo hadi kipa wao kabla ya kuukwamisha wavuni.

Mechi hiyo ilikuwa ni kali nay a kuvutia huku Mgambo kutoka Tanga wakionyesha soka la kuvutia.

Ushindi huo, umeifanya Simba iwe imeshinda mechi tatu mfululizo kati ya nne ilizokuwa imebakiza. Mechi ya mwisho ni mei 18 dhidi ya Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic