Na
Mwandishi Wetu
UONGOZI wa
Simba umechukua uamuzi wa kumpandisha kizimbani kiungo mshambuliaji, Mrisho
Ngassa kutokana na uamuzi wake wa kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea
Yanga.
Ngassa
aliyekuwa akiichezea Simba kwa mkopo kutoka Azam FC, amesaini mkataba wa miaka
miwili kuichezea Yanga lakini Simba wamesema walishasaini naye mkataba wa mwaka
mmoja.
Habari za
uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa, Msimbazi wameamua kufanya mambo
yao kimya na wameamua kutumia mahakama ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.
“Hakika
sasa tumeona suala hili si la kufanya kama filamu, maana wenzetu (Yanga) pamoja
na Ngassa wameamua kutufanyia uhuni. Wachezaji wanataka kufanya Simba ni kama
sehemu ya kuchota fedha na kuondoka.
“Kitu
kibaya zaidi tumegundua system (mfumo) ya soka imekuwa ikiwalinda sana kutokana
na ushabiki mkubwa uliopo katika kamati zilizo chini ya TFF. Sasa sisi tumeona
bora kuchukua hatua zaidi,” kilieleza chanzo cha uhakika.
“Tutamfikisha
Ngassa mahakamani, tutadai zaidi ya Sh milioni 200 kama sehemu ya kutaka fidia
kutokana na mkataba tulioingia. Mkataba upo, msione tumekaa kimya mnaona kama
hatuna cha kusema.
“Ila sasa
tumeamua kufanya mambo kwa mfumo tofauti na leo (jana) usiku tutakuwa na
mkutano kwa ajili ya kujadili kuhusiana na suala hili na tutajua lini rasmi
apande kizimbani.”
Championi
Jumatano ndiyo lilikuwa la kwanza kuandika kuhusiana na Ngassa kusaini Yanga
miaka miwili na kueleza kila anachopata katika mkataba wake, achana na wale
waliosema katika stori yao eti anatarajia kusaini.
Kwa mujibu
wa chanzo hicho kutoka ndani ya Simba, mkataba kati ya Ngassa ulipelekwa na
kusajiliwa TFF tangu Desemba, mwaka jana.
Lakini
baadaye Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope
akathibitisha kuwa mkataba huo tayari waliuwasilisha TFF na kugongwa mhuri.
Suala la
Ngassa kutua Yanga limezua gumzo kubwa na huenda likazua mgogoro mkubwa baina
ya timu hizo mbili.
Blogu hii
ilikuwa ya kwanza kuandika kuhusiana na kiungo huyo kujiunga na Yanga akitokea
Simba.
Mwishoni
mwa mwaka jana, Ngassa alitua Simba kwa mkopo akitokea Azam, lakini
akakabidhiwa gari aina ya Toyota Verossa na Sh milioni 30 na Simba kutangaza
imemuongezea mkataba wa mwaka baada ya kumalizika kwa mkopo, lakini Ngassa
mwenyewe amekuwa akisisitiza hana mkataba na Msimbazi baada ya ule wa Azam.
SOURCE: CHAMPIONI.
0 COMMENTS:
Post a Comment