Kuonyesha kwamba
mechi ya keshokutwa haichukuliwi kiutani, kundi la Friends of Simba limeingia
mzigoni baada ya kutua mjini Zanzibar.
Friends of
Simba wametua mjini Zanzibar mchana huu wakiongozwa na
Mwenyekiti,
Zacharia Hans Pope tayari kufanya mikakati zaidi ya ushindi dhidi ya Yanga
keshokutwa Jumamosi.
Mmoja wa
marafiki hao wa Simba amesema: “Tumefika Zanzibar, baada ya kufika tumepishana
na timu inakwenda mazozini.
“Lakini
jioni tutazungumza na vijana kwa ajili ya kupata dira, kwa kifupi tunataka
kushinda mechi.”
Friends of
Simba na uongozi wa Simba walikutana jana usiku baada ya mkutano wa kwanza
kukwama baada ya Mwenyekiti Ismail Aden Rage kushindwa kutokea.
Timu hizo
zinakutana katika mechi hiyo ya kufunga dimba la Ligi Kuu kila moja ikiwa na
malengo yake.
Yanga
ambayo tayari ni bingwa inataka kulipa kisasi cha mabao 5-0 huku Simba ikitaka
heshima tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment