Tiketi kwa ajili ya pambano la Ligi
Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Yanga litakalochezwa keshokutwa (Jumamosi)
kwenye Uwanja wa Taifa zitaanza kuuzwa kesho (Ijumaa) kwenye vituo mbalimbali
jijini Dar es Salaam.
Vituo vitakavyouza tiketi hizo
kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni ni Uwanja wa Taifa, mgahawa wa Steers
ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, OilCom
Ubungo, kituo cha mafuta Buguruni, BMM Barbershop Sinza Madukani, Dar Live
Mbagala na Sokoni Kariakoo.
Tiketi hizo zitakuwa zikiuzwa katika
magari maalumu yaliyoegeshwa katika vituo hivyo. Viingilio katika mechi hiyo ya
kufunga msimu ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani, sh. 7,000 viti vya bluu, sh.
10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B n ash.
30,000 kwa VIP A.
0 COMMENTS:
Post a Comment