May 23, 2013




Kiungo nyota wa Borussia Dortmund ameamia na ataukosa mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, kesho Jumamosi.

Tayari Dortmund wamethibitisha kuumia kwa Gotze na kwamba ataukosa mchezo huo wa fainali dhidi ya Bayern Munich kwenye Uwanja wa Wembley jijini London.

Mashabiki wa Dortmund wamekuwa na hasira na Gotze licha ya kuwa staa na msaada mkubwa kwa timu hiyo kwa miaka mitatu sasa.


Wameonyeshwa kukerwa kutokana na uamuzi wake wa kuhamia Bayern Munich ambao ni wapinzani wao wakubwa, pia ndiyo watakaocheza nao fainali.

Gotze alishaahidi kwamba angecheza mchezo huo wa fainali kwa kujituma na kuisaidia Dortmund kutwaa ubingwa.
Tayari kumekuwa na taarifa za kwamba hata kuumia kwake inaweza kuwa ni ‘magumashi’ ili kuepuka asicheze fainali hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic