Rais wa zamani wa Real Madrid, Ramon Calderon ameanzisha
mjadala mpya baada ya kusema mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo
ana nafasi kubwa ya kumfuata kocha wake wa sasa Jose Mourinho atakapojiunga na Chelsea.
Tayari Mourinho amethibishwa kuwa atajiunga na
Chelsea na Ronaldo amekuwa kati ya wachezaji anaowataka kuungana nao na kufanya
nao kazi pamoja.
Ronaldo, 27, imeelezwa dau lake linabaki kuwa pauni
milioni 80, fedha walizolipa Real Madrid kumchukua kutoka Man United.
Baada ya kauli ya rais huyo, inaonyesha wazi ndoto
za Ronaldo kurudi Man United zimeyeyuka na sasa Chelsea, PSG na Man City ndiyo
zinaopewa nafasi ya kumchukua.
Kuna taarifa, Chelsea wameshaanza mazungumzo na
Real Madrid na rais huyo amekuwa wa kwanza kutoa siri na mwenyewe amethibitisha
huenda baada ya wiki moja kila kitu kikawa hadharani kama Ronaldo atabaki au
kuondoka.
Tayari Mourinho ameshaagiza mazungumzo yafanyike
kumnasa Wayne Rooney wa Man United na Cavani wa Napoli.
Ronaldo amewahi kulalama kwamba hana raha Madrid,
lakini baada ya mazungumzo na uongozi alirejea katika hali yake na kucheza soka
safi.
Hivi karibuni ilielezwa kwamba yuko katika
mahusiano mabaya na Mourinho, lakini yeye akakanusha.
0 COMMENTS:
Post a Comment