Mchezo wa soka unapendwa kweli kuliko
yote duniani, vijana wako tayari hata kuyatoa maisha yao ili waone mechi za
soka.
Hii ilikuwa mwezi mmoja uliopita wakati
Yanga ilipokwenda mjini Morogoro kuivaa Polisi ya mkoani humo kwenye Uwanja wa
Jamhuri.
Kijana unayemuona hakujali hata kama
anahatarisha maisha yake na badala yake akatembea kama ninja ukutani hadi
alipofanikiwa kuingia ndani.
Hii ni zaidi ya kuruka ukuta na inataka
mazoezi ya kutosha, lakini ameonyesha uwezo mkubwa maana hata wanaoigiza muvi
kule Hollywood wanahitaji vifaa mahsusi ili wacheze michezo kama aliocheza
yeye. Labda Jack Chain peke yake ndiye anaweza, duh!
0 COMMENTS:
Post a Comment