Wakati joto la mechi ya Ligi Kuu
Bara kati ya mechi ya Simba na Yanga likizidi kupanda, Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) limetangaza waamuzi wa mchezo huo.
Mwamuzi wa mechi hiyo atakuwa Martin
Saanya kutoka Morogoro ambapo atasaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha, na Jesse
Erasmo kutoka Morogoro. Mwamuzi wa akiba ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa
Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor)
ni Leslie Liunda.
Hata hivyo, awali mwamuzi alikuwa
Israel Nkongo lakini TFF imechukua uamuzi wa kumbadili baada ya gazeti la
Championi kuandika mapema na kumhusisha na kumlima kadi nyekundu kiungo wa
Yanga Haruna Niyonzima katika mechi dhidi ya Azam FC iliyozya tafrani kubwa
msimu uliopita.
Taarifa nyingine zinasema mwamuzi
huyo amebadilishwa kutokana na kuwa na taarifa za ‘mchezo mchafu’ ambazo yeye
alizishitukia na kukataa kupokea fedha kwa ajili ya kuibeba timu moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment