Hatimaye mashabiki wa Manchester United wamepata bahati ya kumuaga kocha mkongwe nchini humo, Alex Ferguson ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa miaka 27.
Dakika chache kabla ya mechi kati ya Man United dhidi ya Swansea kwenye Uwanja wa Old Trafford, Ferguson aliingia uwanjani na kuwaaga mashabiki hao ambao walikuwa wakimpungia mkono na kumshangilia kwa nguvu.
Baada ya hapo aliwasalimia mashabiki na kuweka saini yake katika vitabu, jezi, mipira kabla ya kwenda kukaa katika mechi na kuanza kushuhudia mechi hiyo dhidi ya Swansea.
Kocha
David Moyes ndiye atachukua nafasi hiyo ya Ferguson na sasa yuko katika Uwanja wa
Goodison Park ambako Everton inapambana na West Ham.
Moyes
naye kabla ya kuanza mchezo huo, aliwaaga mashabiki wa Everton ambao amefanya
nao kazi kwa miaka zaidi ya sita.
0 COMMENTS:
Post a Comment