May 12, 2013




Ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mgambo JKT, umeihakikishia Azam FC kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho tena msimu ujao.

Azam imefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara leo kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar.


Ushindi huo umeifanya Azasm FC ifikishe pointi 51 ambazo haziwezi kufikiwa na Simba wala Kagera wakati mabingwa Yanga tayari wana pointi 55.

Katika mechi hiyo ya leo, Azam walipata mabao yao kupitia John Bocco katika dakika ya 23 na likadumu hadi mapumziko.

Raia wa Ivory Coast Kipre Tchetche alifunga bao la pili dakika ya 66 kabla ya Mkenya Humprey Mieno kufunga la tatu katika dakika ya 80.

Msimu huu Azam FC ndiyo walikuwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Caf na imetolewa na FAR Rabat ya Morocco lakini kabla ilionyesha ushindani mkubwa ikiwa ni pamoja na kuzitoa timu kutoka Sudan Kusini na Liberia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic