Mechi ya mwisho Yanga na Simba kukutana ilikuwa Oktoba 3, 2012 katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, matokeo yalikuwa 1-1.
Vikosi vitakavyoanza leo vinaonyesha vitakuwa havina tofauti kubwa na mechi hiyo ya mwisho.
Saa tatu
baadaye zitaonyesha kazi kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam katika
mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki kwa kuwa itafunga msimu na
Yanga inataka kulipa kisasi cha mabao 5-0 waliyofungwa wakati wa kufunga msimu.
Yanga iliyoanza Oktoba 3,2012 |
Taarifa zinasema, Simba itaanza langoni na kipa Mganda, Abel Dhaira wakati Yanga itaanza na Ally Mustapha ‘Barthez’.
List ya makocha Milovan Cirkovic (Simba) na Ernie Brandts (Yanga) walivyopanga Oktoba 3,2012 |
Kama itakuwa hivyo, maana yake, timu hizo zitakuwa zimebadilishana na Yanga itaanza na kipa wa nyumbani na Simba wa kigeni wakati msimu uliopita zilikuwa tofauti kwa kuwa Yanga ilianza na Yaw Berko raia wa Ghana.
Wachezaji wengine watakaokosa mechi ya leo na walianza mechi iliyopita upande Simba ni Juma Nyosso na Paul Ngalema ambao wamesimamishwa.
Kwa upande wa Yanga, inaonekana wote wapo isipokuwa Berko tu na itategemea na upangaji wa timu kutoka kwa kocha Ernie Brandts.
Penalti:
Mkwaju mmoja wa penalti ulipatikana katika mechi hiyo baada ya Said Bahanuzi kufunga bao la kusawazisha. Je, leo utatokea mkwaju tena?
Kadi nyekundu:
Yanga ilipata pigo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 baada ya kiungo wake wa pembeni, Simon Msuva kulambwa kadi nyekundu.
0 COMMENTS:
Post a Comment