Klabu
za TP Mazembe na Azam FC zimetoa wachezaji wawili kila moja watakaowania tuzo
ya mchezaji bora wa mwaka 2012 ambazo huandaliwa na Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (Taswa).
Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu kutoka Mazembe, John Bocco na Mcha Hamis kutoka
Azam FC wakati Yanga imemtoa Kelvin Yondani na Simba ni Shomari Kapombe
aliyeshinda tuzo hiyo tuzo zilizopita.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Taswa iliyotolewa leo inaeleza hivi:
Kamati
ya kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2012 zinazotolewa na
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imepokea mapendekezo
ya majina ya wanamichezo kutoka vyama mbalimbali kwa ajili ya kuwania tuzo hizo
kwa kila mchezo.
Majina
ya wanamichezo hao yamependekezwa na vyama husika, isipokuwa mpira wa miguu kwa
wanaume pamoja na mpira wa kikapu, ambapo majina yameteuliwa na kamati kwa
kushirikiana na baadhi ya wahariri wa habari za michezo na wadau wa michezo
husika, ingawa awali vyama hivyo viliombwa kuwasilisha majina lakini
havikutekeleza ombi hilo hivyo kamati ikaamua kutafuta utaratibu mwingine wa
kupata majina.
Pia
vyama viwili vya michezo ya paralimpiki na baiskeli bado majina
hayajaifikia kamati yetu kutokana na sababu mbalimbali na tayari wameahidi
watawasilisha majina hayo kabla ya Mei 12 mwaka huu. Chama cha Mpira wa Wavu
pia kimeshindwa kuwasilisha majina.
Hatua
ya mwisho ambayo itafanyika baada ya kupokea mapendekezo hayo kwenye kila
mchezo, Kamati ya Tuzo za Taswa itafanya uchambuzi kupitisha majina hayo
kulingana na sifa ambazo vyama husika vimeleta kwa kila mwanamichezo na kuona
kama wanastahili kupewa tuzo kulingana na vigezo vya kamati na TASWA.
Awali
TASWA ilipanga tuzo hizo zifanyike Aprili 27 mwaka huu, lakini imeshindikana
kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwa nje ya uwezo wa Kamati ya Tuzo pamoja
na chama kwa ujumla na sasa sherehe zitafanyika mwanzoni mwa mwezi Juni katika
tarehe itakayotangazwa baada ya kukubaliana na wadhamini, ambapo mazungumzo
yanatarajiwa kukamilika kabla ya Mei 15 mwaka huu.
Tunavishukuru
vyama vyote vilivyotupa ushirikiano kwa hatua ya awali kwa kutupatia
mapendekezo yao pamoja na kutaja sifa kwa kila mchezaji waliyewasilisha jina
lake nasi tunaahidi tutapitia kwa umakini mapendekezo hayo, lakini uamuzi wa
kamati ndiyo utakaokuwa wa mwisho.
TASWA
itatoa tuzo kwa kila mchezo ambao kamati yetu ambayo Katibu wake ndiye
pia Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando itajiridhisha wanastahili, ambapo baadaye
washindi wa kila mchezo watawania Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa
Mwaka 2012.Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2011 ilienda kwa
Shomari Kapombe. Washindi wengine kwa miaka ya karibuni ni Mwanaidi Hassan
(2010 na 2009), Mary Naali (2008), Martin Sulle (2007) na SMajina ya wanaowania
kwa mwaka 2012:
MPIRA
WA MAGONGO-WANAUME
1
Sylvester Kigodi
2.
Casto Mayuma
3.
Gurtej Bilu Singh
4.
Vendri Bhamra
5.
Elias Samala
Gofu ya
Kulipwa
1 Hassani
Kadio
2 Yassin Salehe
3
Fadhili Nkya
4
Salimu Mwanyenza
5
Rajabu Iddy
GOFU YA
RIDHAA WANAWAKE:
1:MADINA
IDDI
2:ANGEL
EATON
3.
HAWA WANYECHE
4.AYNE
MAGOMBE
GOFU
YA RIDHAA WANAUME
Jimmy Mollel
|
Frank Roman
|
Nuru Mollel
|
Martin MacDonald
|
John Said
|
NGUMI ZA
RIDHAA-WANAUME
1.
Ismail Isack Galiatano
2.
Said Hofu
3.
Selemani Kidunda.
4.
Victor Njaiti
5.
Mohamed Chibumbui.
NGUMI ZA RIDHAA WANAWAKE:-
1. Sara Andrew
2. Irene Kimaro
3. Easter Kimbe.
4. Mather George
5. Mariam Nyerere.
Ngumi za
Kulipwa
1.
Francis
Miyeyusho
2.
Ramadhan
Shauri
3.
Thomas
Mashali
4.
Said
Mbelwa
5.
Francis
Cheka
JUDO-TANZANIA
BARA-WANAUME
1) AHMED
MAGOGO
2) ADREW
THOMAS MLUGU
3) GEOPHREY
EDWARD MTAWA
4) GERVAS
LEONARD CHILIPWELI
5) ABUU
SELEMANI MCHETEKO
6) ABUUBAKAR NZIGE
JUDO
TANZANIA BARA WANAWAKE
1. MATRIDA
.H. TEMBA
2. AMINA
MOHAMED
JUDO ZANZIBAR-WANAUME
1. MOHAMMED
KHAMIS JUMA
2. MASOUD
AMOUR KOMBO
3. MBAROUK
SULEIMANI SULEIMAN
JUDO ZANZIBAR-WANAWAKE
1.
GRACE
ALPHONCE
2.
LAYLATI
MOHAMMED
TENISI-WANAWAKE
[1]
Rehema Athumani
[2]
Vailety Petar
[3]
Mkunde iddi
[4]
Edna John
[5]
Zuhura Baraka
TENISI
Wanaume
[1]
Omary Abdalah
[2]
Yassini Shabani
[3]
Hassan Kasimu
[4]
Kiango Kipingu
[5]
Lebric Jacobu
MPIRA WA
MIKONO-WANAUME
Faraji Shaibu
|
Nyuki ZANZIBAR
|
Hemedi Salehe
|
JKT
|
Abinery Kusena
|
JKT
|
Ally Khamis
|
Ngome
|
Hassani Yusufu
|
Magereza
|
MPIRA WA MIKONO-WANAWAKE
Catherine Mapua
|
Ngome
|
Dorisi Mangara
|
Magereza
|
Zakia Mohamed
|
Ngome
|
Happy Mahinya
|
JKT
|
Mary Kimiti
|
Magereza
|
RIADHA-WANAWAKE
1.Zakia
Mrisho
2.
Mary Naali
3.Jacklin
Sakilu
4.Sarah
Ramadhani
5.Anjelin Tsere
5.Anjelin Tsere
6.
Sara Maja
RIADHA-WANAUME
1.
Dickson Marwa
2.
Faustine Musa
3.
Augstino Sule
4.
Bazil John
5.
Samson Ramadhan
KRIKETI-WANAUME
1. Abhik Patwa.
2. Benson
Mwita.
3. Sefu
Khalifa.
4. Issa
Kikasi.
5. Riziki Kiseto
KRIKETI-WANAWAKE
Monica Pascal.
Mwanaiddi Ibrahim.
Hadija Nasibu
Esther Wales
Mwanaidi Ammy
SOKA-WANAWAKE
FATUMA MUSTAPHA
ASHA
RASHID
MWANAHAMISI
OMARY
SOPHIA
MWASIKILI
ESTER
CHABRUMA
SOKA-WANAUME
JOHN
BOCCO-AZAM
KELVIN
YONDANI-YANGA
SHOMARI
KAPOMBE-SIMBA
MCHA
KHAMISI-AZAM
MBWANA
SAMATTA-TP MAZEMBE
Thomas
Ulimwengu-TP Mazembe
WACHEZAJI
WA NJE WANAOCHEZA TANZANIA
EMMANUEL
OKWI-SIMBA(SASA ETOILE DU SAHEL)-SOKA
KIPRE
TCHETCHE-AZAM-SOKA
HARUNA
NIYONZIMA-YANGA-SOKA
HAMISI
KIIZA-YANGA-SOKA
MARY
WAYA-FILBERT BAYI –NETIBOLI (ALIKUWA KOCHA MCHEZAJI)
KIKAPU-WANAWAKE
Faraja
Malaki- Jeshi
Evodia
Kazinja-JKT Stars
Sajida Ahmed-Don Bosco
Rehema Kilomba-Donbosco
Tukusubira David-Vijana Queens
KIKAPU-WANAUME
Mussa
Chacha-Savio
Lusajo
Samuel Mwakipunda-Oilers
Salim
Mchemba-ABC
Filbert
Mwaipungu-ABC
Steven
Atanasio-ABC
NETIBOLI
Lilian
Sylidion-Filbert Bayi
Mwanaidi
Hassan-JKT
Irene Elias Kanile-Filbert Bayi
Jacqueline Sikozi-Filbert Bayi
Faraja Malaki-Jeshi Stars
WACHEZAJI
BORA CHIPUKIZI
Salum Abubakari-Azam-soka
Frank Domayo-Yanga-soka
Edward
Cristopher-Simba-soka
Emmanuel
Malya-Tenisi Gymkhana Arusha
Tambwe
Juma-Kriketi
WATANZANIA WANAOCHEZA NJE
Mbwana
Samatta-TP Mazembe
Ivo
Mapunda-Gor Mahia
Hasheem
Thabeet-Oklahoma
Thomas
Ulimwengu-TP Mazembe
Soud
Abdulrazak-Uganda (kikapu)
Mohammed
Abdallah ‘dulah’-Uganda (kikapu)
TUZO
YA HESHIMA--- ITATANGAZWA UKUMBINI
TUZO
YA MWANAMICHEZO BORA MWAKA 2012- ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA
MCHEZO
Samson
Ramadhan (2006).
0 COMMENTS:
Post a Comment